logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond aonyesha ubabe katika tamasha za Tuzo za Trace kwa kuwasili na magari ya kifahari

Diamond aliyasafirisha magari hayo kwa mwendo mrefu ikiwemo kuyavusha majini ili kuyafikisha kwenye eneo la tamasha na kuyaegesha kwenye lango la kuingilia ukumbini.

image
na Japheth Nyongesa

Mastaa wako27 February 2025 - 16:25

Muhtasari


  • Kando na matukio ya Trace Awards, hili pia limekuwa likizungumziwa sana na watu mbali mbali wakiwemo wasani wenzake.
  • Mmoja kati ya waandishi wa Diamond naye ameeleza kwamba mari yameekwa hapo kama kivutio  kwa wageni kwani wengi wao wanafika hapo hapo kupiga picha na kujifurahisha.

Mwanamziki wa bongo Tanzania Diamond Platinumz aliamua kupamba tamasha la tuzo za ' Trace ' kwa kuyatumia magari yake ya kifahari.

Inasemekana Diamond aliyasafirisha magari hayo kwa mwendo mrefu ikiwemo kuyavusha majini ili kuyafikisha kwenye eneo la tamasha na kuyaegesha kwenye lango la kuingilia ukumbini.

Kando na matukio ya Trace Awards, hili pia limekuwa likizungumziwa sana na watu mbali mbali wakiwemo wasani wenzake.

Baadhi ya wasani ambao wamezungumzia hili ni pamoja na bosi wa Konde Gang msanii Harmonize. Kwa upande wake alionekana kufurahishwa na hili na kumpa heko mwanamziki mwenzake kupitia video alipowasili na kuyapata magari hayo langoni.

"Napenda ndugu yangu, hili nalo ni zaidi, bro ameamua kutununulia mapanga ni kama anatutisha. Ameamua kuitisha Afrika kwamba amekuja kwenye Trace... bwana kumbe hizi zinavuka. yaani lazima kila atakayefika kwenye hii nchi atajua kuna Simba Dangote,' alisema Haemonize huku akifwatisha kicheko kikubwa

Nandy Mwanamziki na Muigizaji maarufu nchini Tanzania pia alimpa kongole Msanii Diamond kwa kuonesha kwamba uwezo anao. Mwanadada huyo alisema kwa vizuri wageni wajue wao kama wasanii wana biashara pia na zinawalipa.

"Sio kinyongo, tunataka vitu hivi viwe vingi ili sisi pia tuoneshe kwamba tuna biashara na biashara inatulipa. naona pale Diamond kasafisha michuma imekaa pale. mgeni akifika akisoma pale 'Simba' , anauliza simba ni nani ? Diamond Platinumz. Kwamba tunaweza na tunaweza kufanya zaidi vile wanaweza fikiria," alieleza Nandy.

Mmoja kati ya waandishi wa Diamond naye ameeleza kwamba mari yameekwa hapo kama kivutio  kwa wageni kwani wengi wao wanafika hapo hapo kupiga picha na kujifurahisha.

"Kutokea Mola, zanzibar hoteli, ukifika hapa, kitu kikubwa kabisa ambacho kimekuwa ni vutio ni haya magari ya msanii Diamond Platinumz ambayo yameegeshwa hapa. Magari haya yamekuwa ni kivutio kikubwa sana kwa wageni wanaofika hapa. Wengine wakipiga picha na kushagaa. magari haya yamevuka maji. alieleza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved